UTATA WA RAP JAY Z NA NAS WAJIRUDIA TENA.

You are currently viewing UTATA WA RAP JAY Z NA NAS WAJIRUDIA TENA.
  • Post category:Burudani

Marapa wakongwe kutoka marekani Jayz pamoja na Nas wanatarajiwa kuachia nyimbo zao mpya ikiwa ni sehemu ya SoundTrack ya (Judas and The Black Messiah).

Wimbo mpya wa Nas utaitwa ‘EPMD’ na Jayz  ataachia wimbo wake aliomshirikisha Nipsey Hussle kabla ya mauti kumfika, ambao ni ‘What it Feels Like’

Kitendo cha wakongwe hao kuachia nyimbo zao tarehe sawa, kinatafsiriwa kuwa mmoja wao ambae ni Jay-Z anataka kuuzima moto wa rapa Nas aliyeanza kutoa taarifa ya kurudi upya kwenye game.

Hata hivyo kwenye mtandao wa Twitter umeibuka mjadala mzito huku mashabiki wengi wakisema kwamba, walijua tu kwamba Jay Z atatangaza tarehe ya kuachia wimbo wake mpya mara baada ya kusikia Nas katangaza na kweli imetokea hivyo.

Mbali na maneno hayo kutoka kwa mashabiki, kwa Upande wa rapa Nas haonekani kukubali kwamba Jayz anamfanyia Mchezo mchafu.

Robert Elim

Robert Elim better known as Mtoto wa Nyumbani Roba is a new shade of light on the mainstream radio scene! He host an Entertainment show called Interact that usually runs every Monday to Friday from 1:00 PM to 4:00 PM and Interact Extra that runs every Saturday from 10:00 AM to 1:00 PM. Follow him on Twitter and Instagram @robertchiwawa