Nyota wa muziki wa rap nchini Tanzania A.Y kupitia ukurasa wake wa Instagram, ame-share picha anayonekana akiwa mbele ya jengo la Interscope Records huko, California nchini Marekani.
Picha hiyo imekuwa miongoni mwa posti za mkali huyo zilizoacha maswali mengi zaidi kwa mashabiki wa muziki Afrika Mashariki.
Mashabiki wengi wamekuwa na kiu ya kutaka kujua kama kuna dili lolote la A.Y na label hiyo kubwa ya muziki Ila mkali huyo hasajema chochote kuhusu picha hiyo hadi sasa.
Interscope Records ni miongoni mwa lebo kubwa za muziki na maarufu duniani, ilianzishwa mwaka wa1990 na Jimmy Lovine pamoja na Ted Field, inamilikiwa na Universal Music Group kupitia chapa yake ya Interscope Geffen A and M.
Lebo hiyo ya muziki inasimamia wasanii wakubwa na maarufu duniani akiwemo; Eminem, Selena Gomez, Kendrick Lamar, Lady Gaga, na Dr. Dre.