Staa wa muziki nchini Uganda Vinka amechukua mapumziko mafupi kwenye muziki.
Hii ni baada ya kujifungua wiki kadhaa zilizopita ambapo alibarikiwa kumpata mtoto wa kike na mpenzi wake wa siku nyingi Nelly Witta.
Msanii huyo ambaye yupo chini ya lebo ya muziki ya Swangz Avenue amechukua mapumziko ya miezi sita kwa lengo la kutoa matunzo kwa mtoto wake.
Hii ina maana kwamba hataonekana mbele ya umma au kutoa muziki hadi mwezi wa Juni mwaka huu.
Ikumbukwe Vinka ambaye hajekuwa akionekana kwa umma na vyombo vya habari kwa miezi kadhaa, alimtambulisha mpenzi wake Nelly Witta kwa wazazi wake mwezi novemba mwaka wa 2020.