LEXSIL AZUNGUMZA KWA MARA YA KWANZA BAADA YA KUIGURA LEBO YA MUZIKI YA “JUST IN LOVE”.

You are currently viewing LEXSIL AZUNGUMZA KWA MARA YA KWANZA BAADA YA KUIGURA LEBO YA MUZIKI YA “JUST IN LOVE”.
  • Post category:Burudani

Msanii wa muziki nchini Lexsil amezungumza kwa mara ya kwanza tangu ajiondoe kwenye lebo ya muziki ya “Just In Love” inayomilikiwa na Otile Brown.

Akiwa kwenye moja ya Interview Lexsil ambaye anafanya vizuri na wimbo wake uiitwao “Your Love” amesema hana ugomvi wowote na Otile Brown ila alihamua kujiondoa kwenye lebo ya “Just in Love” kwa ajili ya kutanua wigo wa muziki wake.

Hata hivyo amemshukuru Otile Brown kwa kumshika mkono kwa miezi sita aliyokuwa chini ya lebo yake ya muziki kwani amejifunza mambo mengi ambayo yatamsaidia kimuziki.

Ikumbukwe Lexsil alisainiwa na Otile Brown kwenye lebo ya “Just in Love” mwezi Septemba mwaka wa 2020 na alifanikiwa kuachia ngoma mbili ambazo ni “Dance Along” na “Remedy” aliyomshirikisha Otile Brown.

Robert Elim

Robert Elim better known as Mtoto wa Nyumbani Roba is a new shade of light on the mainstream radio scene! He host an Entertainment show called Interact that usually runs every Monday to Friday from 1:00 PM to 4:00 PM and Interact Extra that runs every Saturday from 10:00 AM to 1:00 PM. Follow him on Twitter and Instagram @robertchiwawa