Socialite maarufu nchini Huddah Monroe amejitokeza wazi na kunyosha maelezo kuhusu madai ya kuwa kwenye bifu na staa wa muziki nchini Tanasha Donna.
Kupitia insta story yake kwenye mtandao wa Instagram Bi Monroe ameweka wazi kwamba hana ugomvi na mtu yeyote kama inavyoripotiwa huku akiwataka wakenya kwenye mitandao ya kijamii kuacha suala la kuwagonganisha wanawake kwa mambo madogo.
Mrembo huyo ambaye ni CEO wa bidhaa za urembo za Huddah ameenda mbali zaidi na kusema kwamba kauli yake kuhusu watu kuwa na wafuasi wengi kwenye mitandao ya kijamii haikumlenga mtu yeyote bali amekuwa akitoa kauli hiyo mara kwa mara.
Kauli ya Huddah Monroe inakuja wakati huu watu wanamtuhumu kwenye mitandao ya kijamii kuwa ana chuki na Tanasha Donna mara baada ya kuwa msanii wa kwanza wa kike nchini kupata wafuasi wengi kwenye mtandao wa Instagram.