Staa wa muziki nchini Uganda Cindy Sanyu ambaye ni Naibu Rais wa Muungano wa Wanamuziki nchini humo (UMA) ametangaza tena kuwania wadhfa wa urais wa muungano huo.
Cindy ambaye alijetenga na masuala ya kuwania urais wa muungano wa wasanii nchini Uganda wiki iliyopita kwa sasa amebadilisha mawazo yake na kuweka wazi kuwa atakuwa miongoni mwa wagombea wa kiti hicho kwenye uchaguzi ujao.
Hata hivyo amesema alichukua uamuzi huo baada ya kuwa na mazungumzo mapana na wadau wa muziki nchini Uganda,ambao walimshawishi kugombea wadhfa wa urais wa muungano wa wasanii nchini humo ambao uliachwa wazi na msanii Ykee Benda ambaye alijiuzulu wiki kadhaa zilizopita.
Cindy anajiunga na wasanii GNL Zamba pamoja na Sophie Nantogo ambao wametia nia ya kuwania wadhfa wa urais wa muungano wa wasanii nchini Uganda.