Staa wa muziki nchini Uganda Chris Evans amefunguka na kusema kwamba ana mpango kufunga ndoa hivi karibuni.
Mkali huyo wa ngoma ya “Sitidde” amedokeza hayo kwenye moja ya interview akisema kuwa amechoshwa na maswali kuhusu maisha yake ya ndoa.
Chris Evans amesema kwa sasa yupo kwenye mahusiano na mwanamke wa ndoto yake, hivyo kila kitu kipo shwari.
Alipoulizwa amtambulishe mwanamke huyo Chris Evans alidinda na kusema kuwa watu watamfahamu hivi karibuni.
Ikumbukwe Chris Evans ni kipenzi cha wanawake wengi nchini Uganda kutokana na sauti yake ya kumtoa nyoka pangoni.