Kundi la muziki wa Gengetone nchini Ochungulo Family limevunjika baada ya kwa nyimbo zao zote kufutwa kwenye mtandao wa Youtube.
Taarifa za kundi hilo kuvunjika zilianza kusambaa mitandaoni jumatano wiki hii wakati akaunti yao ya youtube yenye wafuasi elfu 158 ilichukuliwa na Nelly The Goon ambaye ni mmoja kati ya members wa Ochungulo Family.
Kundi la Ochungulo Family ambalo lilikuwa linaundwa na wasanii Benzema, Nelly The Goon na Dmore halijeweka wazi sababu za kuafikia uamuzi huo ila wajuzi wa mambo wanahisi kwamba huenda wasanii wa kundi hilo wamekuwa na mgogoro wa kugawa mapato na ndio chanzo cha kuvunjika kwake.
Ikumbukwe wasanii wa Ochungulo Family wamekuwa wakifanya kazi kama wasanii wa kujitegemea huku wakishirikishwa na wasanii kwenye kazi zao kabla ya kuafikia uamuzi wa kulivunja kundi hilo.