PRODYUZA DIGI BAUR AKANA MADAI YA KUMROGA MSANII JOSE CHAMELEONE.

You are currently viewing PRODYUZA DIGI BAUR AKANA MADAI YA KUMROGA MSANII JOSE CHAMELEONE.
  • Post category:Burudani

Mwaka wa 2020,mtayarishaji wa muziki nchini Uganda, Diggy Baur alitishia kumroga msanii Jose Chameleone baada ya msanii huyo kumpiga na kumjeruhi vibaya.

Diggy Baur alisema atawasiliana na mababu zake ili Chameleone asishinde kiti cha umeya wa jiji la Kampala kwenye uchaguzi mkuu uliyokamilika majuzi nchini Uganda.

Siku ya Jumatano wiki iliyopita, Chameolene alishindwa na Erias Lukwago ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka wa 2021 na kutokana na hilo msanii huyo ameonekana kuwa na huzuni.

Diggy Baur sasa amejitokeza na kujitenga na madai ya kumroga  Jose Chameleone kama alivyoahidi kwenye video iliyosambaa mitandaoni.

Hata hivyo Chameleone bado yupo kimya juu ya jambo hilo lakini pia hajejitokeza kuzungumzia suala la kushindwa kwake kwenye uchaguzi wa umeya wa jiji la Kampala.

Ikumbukwe Chameleone alimpiga prodyuza huyo kama mwizi wa kuku lakini wawili hao walikuja wakaweka tofauti zao baada ya kurushiana maneno makali kwenye mitandao ya kijamii.

Robert Elim

Robert Elim better known as Mtoto wa Nyumbani Roba is a new shade of light on the mainstream radio scene! He host an Entertainment show called Interact that usually runs every Monday to Friday from 1:00 PM to 4:00 PM and Interact Extra that runs every Saturday from 10:00 AM to 1:00 PM. Follow him on Twitter and Instagram @robertchiwawa