Nyota wa muziki wa Bongofleva, Whozu amekemea vikali picha inayo sambaa mitandaoni ya watu wawili wanaohisiwa kuwa ni wapenzi, mwanaune pichani akihusishwa kuwa ni yeye.
Picha hiyo mara ya kwanza aliipost aliyekuwa mke wa harmonize Sarah kwenye insta story yake kwenye mtandao wa Instagram, huku tafsiri ikiwa ni mwanaume mpya wa mwanadada huyo ambaye ni mtalaka wa msanii Harmonize.
Mwanaume huyo ambaye haonekani sura kwenye picha hiyo anahusishwa kuwa ni Whozu, kitu ambacho kimeleta tafsiri ya kuwa wawili hao wapo katika mahusiano kulingana na aina hiyo ya picha.
Whozu kupitia ukurasa wake wa Instagram, amenyoosha maelezo kwa staili hii, “Kwa hivyo siku hizi mimi nina hips? Kwamba MTU akivaa nguo ya juu nyie mnampa viatu? Acheni hizo mkoje”.