Staa wa muziki nchini Uganda Mary Bata amethibitisha kumsajili msanii wa kike nchini humo Kemi Sera kwenye lebo yake ya muziki ya MBM.
Bata ameweka wazi hilo kwenye moja ya interview ambapo amesema ana imani na Kemi ambaye alipoteza dira kimuziki kutokana na matumizi ya mihadarati.
Aidha amesema amehamua kumpa Sera nafasi nyingine kukuza kipaji chake ambacho anadai karibu kipotea kutokana na uraibu wa madawa za kulevya.
Ikumbukwe miezi kadhaa zilizopita kemi Sera alikuwa anapitia wakati mgumu kwenye maisha yake baada ya kupatwa na msongo wa mawazo jambo lilomfanya ajitokezee na kuzungumzia hali yake ambapo alisema kuwa meneja wake wa zamani Hajji Haruna alikuwa anamnyanyasa kingono.
Hata hivyo ni madai ambayo yalipuziliwa mbali na Hajji Haruna ambaye alisema kwamba anawaheshimu wanawake wote na hawezi kuwadhulumu kimapenzi.