Wiki iliyopita Jay-Z aliingia kwenye headlines za dunia kwa kuuza hisa nyingi za mtandao wake wa TIDAL kwa kampuni ya SQUARE ambayo inamilikiwa na Jack Dorsey, CEO wa Twitter.
Jay-Z ambaye alikuwa mmiliki wa mtandao huo aliingiza takribani TSh. Bilioni 32.5. Licha ya Jay Z kumiliki TIDAL, kuna wasanii ambao pia wana hisa zao kwenye mtandao huo, akiwemo Rihanna, Beyonce, J. Cole, Nicki Minaj, T.I , Kanye West na wengine.
Sasa imeripotiwa kuwa wasanii hao nao wamefaidika na mauzo hayo kwani wamepatiwa 3% ya mauzo ambapo kila mmoja ametia kibindoni takribani millioni 976, huku pia wakiendelea kuwa na hisa zao kama kawaida.