Rapa kutoka nchini Marekani Bobby Shmurda ameachiwa uhuru kutoka gerezani baada ya kutumikia kifungo chake tangu mwaka wa 2014.
Kupitia ukurasa wa Instagram wa rapa Bobby Shmurda imepostiwa video kutambulisha ujio wake mtaani, ikiwa ni miaka takiribani saba imepita tangu afungwe.
Mkali huyo wa ngoma ya “Hot Nigga”, mwaka wa 2016 alihukumiwa kifungo cha miaka 7 jela kufuatia kuhusishwa na mauaji.
Bobby alinyimwa msamaha na maofisa wa ‘Parole’ septemba mwaka 2020 na ikambidi aendelee kutumikia kifungo hadi Disemba 11, mwaka wa 2021.
Lakini kamati ya time Allowance Committee ilitengua maamuzi ya maofisa wa Parole na kuruhusu kifungo cha Bobby Shmurda kumalizika Februari 23 mwaka huu.
Baada ya kuachiwa huru ataendelea kuripoti kwa maofisa wa Parole hadi mwaka wa 2026.