Rapa kutoka nchini uganda Gravity Omutujju amekanusha madai yanayosambaa mitandaoni kwamba alitumia pesa alizolipwa na chama cha Kiusiasa cha NRM kujenga mjengo wake wa kifahari ambao alishare kwa mashabiki zake majuzi.
Akipiga stori na radio moja nchini Uganda Omutujju amekana madai hayo na kusema kuwa mjengo wake huo umetokana na bidii pamoja na juhudi zake mwenyewe,
Aidha ametumia fursa hiyo kuwashauri wasanii wa muziki nchini uganda kuwekeza kwenye vitu vitakavyowapa faida ya kujiendeleza kimaisha badala ya kutumia pesa zao kwenye shughuli za starehe.
Kauli ya Gravitty Omutujju inakuja mara baada ya wajuzi wa mambo nchini Uganda kudai kwamba alilipwa shillingi millioni 5.9 na chama cha kisiasa cha NRM, hivyo alitumia pesa hizo kujenga mjengo wake huo wa kifahari.