Staa wa muziki wa BongoFleva kutoka label ya WCB Mbosso ameachia Cover rasmi ya Album yake ya “DEFINITION OF LOVE”.
Album hiyo inayosubiriwa kwa Hamu na mashabiki wa muziki mzuri mashariki inatarajiwa kuachiwa rasmi machi 13 mwaka huu 2021.
Mbosso bado hajaweka wazi idadi ya Ngoma zitakazopatikana kwenye Album hiyo na ni wasanii gani wameshiriki kuikamilisha album ya Definition Of Love.
Mashabiki Wategemee Kazi Nzuri kutoka kwa Mbosso hii ikiwa ni Album yake ya kwanza tangu aianze safari yake ya Muziki.