Mwanamuziki wa nyimbo za injili nchini Wahu amejibu juu ya madai yaliyoibuliwa na baadhi ya wakenya kwenye mitandao ya kijamii kuwa amerudi kwenye muziki wa kidunia mara baada ya kuuachia wimbo wa mapenzi.
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa instagram Wahu amefunguka na kusema kwamba hajutii kutunga wimbo wa mapenzi uitwao “This Love Ya Wahu” kwani kufanya hivyo sio dhambi.
Aidha amesema katika maisha suala la mapenzi limetawala, hivyo kitendo chake cha kutunga wimbo wa mapenzi hakiendi kinyume na imani yake huku akisisitiza kwamba hajeacha kumtumkia Mungu.
Ikumbukwe wahu alitangaza kuacha muziki wa kidunia mwaka wa 2017 na kuhamia kwenye muziki wa injili mara baada ya kuachia wimbo wake uitwao “Sifa.”