Msanii wa kike anayechipukia kwenye muziki wa Gengetone nchini amejitokeza na kudai kwamba ana mimba ya Staa wa muziki nchini Willy Paul.
Mrembo huyo ambaye anafahamika kama “Dee” amedai kwamba Willy Paul amemkimbia tangu ampe uja uzito, hivyo amehamua kuweka wazi masaibu yake ili mtoto wake atakayezaliwa apate malezi kutoka kwa msanii huyo.
Hata hivyo Willy Paul hajetoa tamko lolote kuhusu tuhuma zilizoibuliwa na mrembo huyo ila wajuzi wa mambo wanahisi kwamba huenda mwanamke huyo amelipwa na Willy Paul kuibua madai hayo ili aweze kuzungumziwa kwenye habari za burudani nchini.