WANAOENDELEZA BIASHARA YA SALUNI NA VINYOZI WAKATI HUU WA MLIPUKO WA CORONA WAONYWA TURKANA

  • Post category:County News

Onyo imetolewa kwa wananchi wanaoendeleza biashara ya vinyozi na saluni katika kaunti ya Turkana kwamba watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Akizunguza mjini lodwar kamishna wa kaunti hiyo Muthama Wambua amesema licha ya serikali kuagiza kufungwa kwa biashara hizo baadhi ya wananchi wamekuwa wakikiuka amri hiyo na huenda wakahatarisha maisha wakati hu virusi vya COVID-19.

Aidha Muthama amasema kwa sasa wanaendeleza mikakati ya kuwahamasisha wananchi kuhusu umuhimu wa kuvalia vitamvua au maski wanapokuwa katika maeneo ya umma sawia na kufuata maagizo yote yanayotolewa na serikali  ili kuepuka na maambukizi ya Corona.

Yanajiri hayo huku wahudumu wa bodaboda kaunti hiyo wakiridhia kufuata maagizo yanayotolewa  na serikali japo wanaitaka serikali kuu kuwasaidia makundi ya watu wasiojiweza wakati huu shughuli nyingi imeathirika kutokana na Corona

Robert Elim

Presenter and News Editor at North Rift Radio Kenya