CHAMA CHA JUBILEE KUWAADHIBU WAWAKILISHI WADI WALIOANGUSHA MSWADA WA BBI.

You are currently viewing CHAMA CHA JUBILEE KUWAADHIBU WAWAKILISHI WADI WALIOANGUSHA MSWADA WA BBI.

Chama cha Jubilee kitawaadhibu zaidi ya Wawakilishi wadi 20 waliopiga kura ya kuuangusha mswada wa marekebisho ya katiba mwaka wa 2020.

Kwa mujibu wa Naibu katibu mkuu wa Jubilee Joshua Kuttuny, wawakilishi wadi hao walipiga kura kinyume na mwongozo wa chama wa kutaka waupitishe mswada huo.

Kuttuny ambaye pia ni mbunge wa Cherenganyi anasema tayari wameanza kupokea malalamishi kutoka kwa magavana wa Jubilee kuhusu utendakazi wa waakilishi hao bungeni akisema wamekuwa wakikosa kuunga mkono miswada inayopendekezwa na chama.

Hata hivyo amedokeza kwamba wawakilishi wadi kaunti ya Nairobi, Elgeiyo Marakwet ni miongoni mwa watakaoadhibiwa kwa kufanya uamuzi binafsi wakati wa kupigiwa kura wa BBI.

Robert Elim

Robert Elim better known as Mtoto wa Nyumbani Roba is a new shade of light on the mainstream radio scene! He host an Entertainment show called Interact that usually runs every Monday to Friday from 1:00 PM to 4:00 PM and Interact Extra that runs every Saturday from 10:00 AM to 1:00 PM. Follow him on Twitter and Instagram @robertchiwawa