Mwakilishi wa akina mama kaunti ya Turkana Joyce Emanikor amekanusha madai yaliyokuwa yakisambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa amekutwa na maambukizi ya virusi vya corona.
Akizungumza na meza yetu ya habari Emanikor amesema madai hayo hayana msingi wowote kwani yuko salama salimini.
Aidha amesema huenda ni njia ambayo imetumiwa na baadhi ya wapinzani wake kumpaka tope huku kutoa wito kwa wanamchi kujitenga na habari za kupotosha kuhusiana na ugonjwa wa corona ambazo zinasambazwa kwenye mitandao.
Hata hivyo amewataka wakaazi wa kaunti ya Turkana waendelee kushirikiana na serikali ya kaunti na ile ya kitaifa katika hatua kukabiliana na ugonjwa huo hatari kwa kuzingatia usafi wa kila mara.