SERIKALI KUU IMETAKIWA KUWEKA MIKKATI YA KUZIPA CHAKULA FAMILIA MASKINI TURKANA

  • Post category:County News

Serikali ya kitaifa imetakiwa kuweka mikakati mwafaka itakayohakikisha wananchi wanaotoka katika familia maskini katika kaunti ya Turkana wanapata chakula wakati huu ambapo serikali imetoa marufuku ya kutotoka nje.

Ni wito ambao umetolewa na wakaazi wa Nakwamekwi viungani mwa mji wa Lodwar ambao wamesema huenda makali ya njaa yawakawaathiri pakubwa baada ya shughuli walizokuwa wakitengemea kama kitega uchumi kusimamishwa kutokana na corona.

Aidha wameitaka mashiriki yasiokuwa ya kiserikali katika kaunti ya Turkana kujitokeza kuwasaidia na misaada ya chakula katika kipindi hiki kigumu cha maambukizi ya virusi vya covid 19.

Kauli yao inakuja baada ya kupokea misaada ya vyakula na bidhaa nyingine kutoka kwa Kundi la wasomi eneo la Nakwamekwi kwa ajili ya kuzisaidia familia ambazo zimeathirika pakubwa na makali ya njaa.

Robert Elim

Presenter and News Editor at North Rift Radio Kenya