WIZI WA MABAVU KATIKA KANISA LA SOLUTION JESUS GLORY,TRANS-NZOIA.

WIZI WA MABAVU KATIKA KANISA LA SOLUTION JESUS GLORY,TRANS-NZOIA.

Viongozi na waumini wa madhehebu mbalimbali kwenye soko la Endebess katika Kaunti ya Trans Nzoia wametoa wito kwa vyombo vya usalama kulisaka genge la wezi ambalo limekuwa likibomoa makanisa na kuiba vifaa vya kieletroniki na vifaa vingine vyenye thamani nyakati za usiku.

Kisa cha cha hivi karibuni kikiwa cha Kanisa la Solution Jesus Glory ambapo Askofu wa Kanisa hilo Michael Barasa anadai kuwa genge hilo lilitoweka na vipaza sauti na kuwaacha waumini wakikadiria hasara ya maelfu ya pesa.

Hata hivyo Barasa ameshangazwa jinsi genge hilo limekuwa likiutekeleza wizi  huo wakati ambapo amri ya Rais Uhuru Kenyatta ya kutopatikana nje usiku ingalipo.

Robert Elim

Presenter and News Editor at North Rift Radio Kenya