Viongozi kutoka kaunti ya Turkana wakiongozwa na gavana wao Josphat Nanok wametaka serikali ya taifa kushughulikia tatizo la ukosefu wa usalama katika eneo la Kapedo katika kaunti ndogo ya Turkana mashariki bila upendeleo.
Haya yanawadia baada ya shambulizi ambayo inasemekana kutekelezwa na majangili kutoka jamii jirani ambapo maafisa wawili wa polisi waliripotiwa kuawa kwa kupigwa risasi.
Akiwahutubia wanahabari mjin Lodwar, Nanok ambaye alikuwa ameandamana na, wabunge james lomenen, Mohammed Ali Lokiru,John Lodepe na viongozi wengine kaunti hiyo wameelezea masikitiko yao juu mauji yanayoendelezwa na majangili eneo la turkana mashariki huku wakisema juhudi za kutafuta amani ya kudumu katika eneo hilo zinatatizwa na baadhi ya viongozi kutoka kaunti ya baringo.
Aidha wameitaka serikali kuu kuendesha operasheni mpakani mwa kaunti ya turkana mashariki na baringo bila upendeleo hadi pale majangili wanaotatiza amani eneo hilo watakaposalimia amri.
Hata hivyo wametolea wito kwa serikali kupitia wizara ya usalama wa ndani kuweka mikakati zaidi ya kupata suluhu la kudumu ili kukomesha uhasama unaoshudiwa mara kwa mara baina ya jamii za wafugaji mpaka mwa kaunti za turkana na Baringo.