Mahakama mjini Kabarnet kaunti ya Baringo imetoa maagizo ya kuzuia mabunge ya seneti na lile la kitaifa kuchukua hatua dhidi ya bunge la kaunti ya Baringo kwa kuangusha mswada wa BBI.
Haya yanajiri baada ya waakilishi wadi wanaoegemea mrengo wa KANU kuwasilisha kesi mahakamani wiki moja iliyopita kupinga matokeo ya kuangushwa kwa mswada huo kwa msingi kwamba haukufuata utaratibu unaohitajika wa kuwahusisha wananchi kupitia mpango wa uhamasisho kabla ya kuwasilishwa bunge.