Zaidi ya watu elfu 70 katika kaunti ya Turkana wamefanya vipimo vya Corona kama njia moja ya kudhibiti kuenea kwa virusi vya covid 19 kaunti hiyo.
Akiongea na meza yetu ya habari Afisa katika Wizara Afya kaunti ya Turkana Dakta Gilchrist Lokoel amesema zoezi hilo lilifanywa kwenye kaunti ndogo zote kaunti hiyo ambapo watu 23,256 wamefanywa vipimo Turkana Kusini,Turkana ya Kati watu 35,884,Turkana Magharibi watu 5,779,Turkana Mashariki watu 2,750, Loima watu 1034 na Kibish watu 44.
Aidha amesema watu wote 72,401 ambao walifanyiwa vipimo wamepatikana hawana maambukizi ugonjwa wa corona ambao unasababishwa na virusi vya covid-19.
Hata hivyo amesema kuwa serikali ya kaunti inaendelea kuweka mikakati kuhakikisha janga la corona linadhibitiwa kwani wahuduma wa afya wametumwa kila kona ya kaunti hii kutoa elimu kwa umma dhidi ya corona.