WANAFUNZI KATIKA SHULE ZA UMMA KUNUFAIKA NA BARAKOA MILLIONI 4

Wanafunzi wote katika shule za umma nchini wanatarajiwa kunufaika na zaidi ya barakoa milioni 4 kutoka kwa Shirika la Kusambaza Dawa nchini KEMSA.

Kulingana na Kaimu Afisa Mkuu wa KEMSA Edward Njoroge mwezi huu wa Februari barakoa zaidi ya laki sita zitasambazwa katika kaunti ya Nairobi, Kiambu na Muranga.

Aidha Njoroge amesema barakoa milioni 3 zimetengwa kwa watoto walio katika shule ya chekechea, walio katika gredi ya nne hadi darasa la nane wakipewa barakoa milioni 2.25 na walio katika shule za upili wakipewa idadi sawia.

Hata hivyo ameongeza kuwa KEMSA imepokea taarifa kutoka kwa Wizara ya Afya kuhusu idadi ya barakoa zinazohitajika katika kila kaunti.

Robert Elim

Robert Elim better known as Mtoto wa Nyumbani Roba is a new shade of light on the mainstream radio scene! He host an Entertainment show called Interact that usually runs every Monday to Friday from 1:00 PM to 4:00 PM and Interact Extra that runs every Saturday from 10:00 AM to 1:00 PM. Follow him on Twitter and Instagram @robertchiwawa