Mabunge ya Kitaifa na ile ya Seneti yametakiwa kuiga mfano wa zile za kaunti na kupasisha upesi mswada wa marekebisho ya katiba mwaka wa 2020 kupitia BBI.
Kinara wa chama cha ODM Raila Odinga ameahidi kuhakikisha kwamba wananchi mashinani wanafaidi kupitia bbi ikizingatiwa kwamba ina manufaa mengi kuliko mapungufu.
Aidha waziri wa ugatuzi Eugine Wamalwa amewataka magavana kuwa mabalozi wa kushinikiza kupasishwa kwa bbi akisema kupitia mpango huwo ugatuzi utaimarika hata zaidi.