Serikali imeendelea kuwaonya vikali wanasiasa ambao wanaotoa jumbe zinazowezakusababisha chuki nchini hasa wakati huu ambapo serikali inajiandaa kwa uchaguzi mkuu ujao
Msemaji wa serikali Kadinali mstaafu Cyrus Oguna amesema idara zinazohusika zinafuatilia kwa makini mienendo ya wanasiasa na watakaopatikana na hatia watachukuliwa hatua kali za kisheria
Kauli ya Oguna inajiri huku idara mbalimbali za serikali ikiwemo Bunge ,Tume ya Uwiano na Utangamano NCIC ,ile ya Uchaguzi IEBC, Tume ya Kukabili Ufisadi EACC na DCI zikisema zitashirikiana kudumisha maadili nchini.