WAZIRI WA MAJI SICILY KARIUKI AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI

You are currently viewing WAZIRI WA MAJI SICILY KARIUKI AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI

Waziri wa maji Sicily Kariuki amezuru Kaunti ya Pokot Magharibi kukagua miradi ya unyinyiziaji maji mashamba ya Chesakat iliyoko eneo bunge la Sigor na Kases eneo bunge la Kacheliba.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kariuki anasema miradi hiyo ni moja kati ya zile ambazo Serikali imeanzisha kusaidia kuimarisha amani mipakani.

Anasema tayari mradi huwo umekamilika kwa asimilia sitini ikilengwa kukamilika kabla ya mwisho wa mwezi machi mwaka huu.

Aidha waziri Kariuki anasema  mradi huwo wa kilimo cha unyunyiziaji maji mashamba utawafaidi zaidi ya wakaazi alfu tatu na kwamba serikali inanuia kuwawezesha wakulima kuhusu maswala ya kilimo na mbinu bora za kuhifadhi maji.

Amewataka wanakandasi ambao wamepewa tenda hiyo kuwa makini wanapojenga bwawa hilo ili kuepuka majanga hapo baadaye.

Alex Toilem

Mwandishi, mhariri na msomaji wa habari Northrift Radio 104.9/104.5FM kapenguria.