Kaunti zilizoko Kaskazini mwa Bonde la Ufa zimepokea dosi alfu 60 za chanjo ya ugonjwa wa COVID-19.
Kaunti ya Uasin Gishu ambako chanjo hiyo inahifadhiwa imepokea dosi alfu 30 ya chanjo hiyo zitakazosambazwa kwa kaunti zote za Kaskazini mwa Bonde la Ufa.
Waziri wa Afya kaunti ya Uasin Gishu Everlyn Rotich amesema wahudumu wa afya, maafisa wa usalama pamoja na walimu katika kaunti hiyo watapokea chanjo hiyo katika vituo vya huruma na hospitali ya rufaa na mafunzo Eldoret ambazo zitapoke dosi alfu 15 na dosi alfu 6 mtawalia.