MBUNGE WA POKOT KUSINI DAVID PKOSING ASUTWA KWA KUTUMIA MIRADI YA SERIKALI KUJITAKIA MAKUU KISIASA.

You are currently viewing MBUNGE WA POKOT KUSINI DAVID PKOSING ASUTWA KWA KUTUMIA MIRADI YA SERIKALI KUJITAKIA MAKUU KISIASA.

Mbunge wa Kapenguria Samuel Moroto amemsuta mwenzake wa Pokot kusini David Pkosing  kwa kuendelea kuwahadaa wananchi kuhusiana na miradi ya ujenzi wa barabara katika maeneo tofauti Kaunti ya Pokot Magharibi.

Kulingana na Moroto licha ya kwamba Pkosing ni mwenyekiti wa kamati ya uchukuzi hafai kutumia fursa hiyo kujitakia makuu kisiasa.

Moroto hata hivyo amemtaka Pkosing kushirikiana na viongozi wengine kaunti hiyo kuboresha maendeleo kando na kuhakikisha umoja wa kaunti badala ya kutaka kujitakia makuu kisiasa.

Alex Toilem

Mwandishi, mhariri na msomaji wa habari Northrift Radio 104.9/104.5FM kapenguria.