MAAFA TURKANA YA KATI BAADA YA MTO KAWALASE KUVUNJA KINGO ZAKE

Watu wawili wamesombwa na mafuriko kaunti ya ndogo ya Turkana ya kati baada ya mto Kawalase kuvunja kingo zake usiku wa kuamkia leo.

Kulingana na waliofika kwenye eneo la mkasa wawili hao   walikutana na mauti yao baada ya gari aina Landcruiser walimokuwa wakisafiria kutoka Lodwar kwenda Kakuma kusombwa na maji ya mto huo.

Wakati huo huo wakaazi wa kaunti ndogo ya Turkana ya kati wameshutumu mwanakandarasi aliyepewa jukumu la kukarabati barabara ya Lodwar-Kakuma kwa kujikokota katika ujenzi wa daraja liloko mto Kawalase  ikizangatiwa mto kuwa huo umesababisha maafa  mengi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa madereva kaunti ya Turkana Maxwel Ekamar amesikitishwa na kisa hicho huku akiwataka madereva kaunti hiyo kuwa makini barabarani hasa wakati huu mvua inaendelea kunyesha ili wasihatarishe maisha yao.

Hata hivyo amesema dereva yeyote katika kaunti ya Turkana atakayepatikana akivuka mito ambayo imefurika kipindi hiki cha mvua atachukuliwa hatua kali za kisheria kwani kwa sasa yupo mbioni kuzungumza na makampuni mbali mbali ambazo zimewaajiri madereva kuhakikisha zinachukua tahadhari msimu huu wa mvua.

Robert Elim

Robert Elim better known as Mtoto wa Nyumbani Roba is a new shade of light on the mainstream radio scene! He host an Entertainment show called Interact that usually runs every Monday to Friday from 1:00 PM to 4:00 PM and Interact Extra that runs every Saturday from 10:00 AM to 1:00 PM. Follow him on Twitter and Instagram @robertchiwawa