WAKAAZI POKOT MAGHARIBI WATAKIWA KUCHUKUA TAHADHARI YA MAFURIKO NA MAPOROMOKO YA UDONGO.

Viwango vya mvua vimekuwa vikiongezeka kila mwaka na kuna madhara makubwa hasa mwaka huu katika maeneo kuliko na miinuka gatuzi la Pokot Magharibi.

Kulingana na Mkurungezi mkuu wa Utabiri wa Hali ya Hewa Pokot Magharibi Wilson Lonyang’ole, ikiwa unaishi kando ya mto Kong’elai, Weiwei, maeneo ya Chesogon na Tamkal uanza kuchukua tahadhari mapema kabla ya hatari kutokana na ujio wa mvua nyingi mwezi machi ambayo itaandamana na mafuriko na hata maporomoko ya udongo

Katika mzungumzo ya kipekee ya North Rift Radio, Lonyag’ole vilevile ametoa tahadhari kwa wakaazi wa maeneo ya Ortum hususan Ortum Center kuchukua tahadhari kutokana na eneo hilo kuwa na mito mitatu na mipasuko ya mikondo ya maji.

Robert Elim

Robert Elim better known as Mtoto wa Nyumbani Roba is a new shade of light on the mainstream radio scene! He host an Entertainment show called Interact that usually runs every Monday to Friday from 1:00 PM to 4:00 PM and Interact Extra that runs every Saturday from 10:00 AM to 1:00 PM. Follow him on Twitter and Instagram @robertchiwawa