Wakaazi wa Napetet kaunti ya ndogo Turkana ya Kati wamefaidi na vifaa vya kujilinda dhidi ya virusi vya Corona vikiwamo mitungi ya kuhifadhi maji,maski na vieuzi kutoka kwa shirika la Practical Action.
Akizungumza baada ya kupokea msaada huo Msimamizi wa mradi katika Shirika la Practical Action Joel Ombok amesema shirika hilo litaendelea kutoa hamasisho kwa jamii kuhusiana na mbinu za kujilinda dhidi ya virusi vya Corona.
Aidha Ombok amesema kama njia moja ya kuwaepusha wananchi kusafiri mwendo mrefu kutafuta maji,shirika hilo linapania kuchimba visima zaidi ya nane katika kaunti ya Turkana.
Wakati huo huo Chifu wa Kata ya Napetet Patrick Lorogoi ameshabikia hatua hiyo akisema imewafaidi pakubwa wananchi ambao hawakuwa na uwezo wa kununua bidhaa hizo msimu huu janga la Corona.