Bodi ya usimamizi za taasisi mbalimbali zimehimizwa kuhakikisha kwamba madereva wanaoajiriwa kuendesha mabasi ya shule ni wale waliokomaa na wenye tajriba ya kuhakikisha wanafunzi wako salama barabarani
Meneja wa eneo Bunge la Kiminini kaunti ya Trans-Nzoia Jackson Muganda anasema hazina za ustawishaji maeneo bunge CDF na ugatuzi imepiga jeki maendeleo ya mashinani kwa kuwawezesha wasimamizi kuimarisha miundo misingi shuleni na vilevile ya kununua mabasi.
Aidha Muganda ameonya kwamba wakuu wa shule watakaokiuka sheria kwa kutumia njia za mkato na kuwaajiri jamaa zao wataadhibiwa kisheria.