Mfanyibiashara mmoja wa nyumba kupanga eneo la Kambi mpya viungani mwa mji wa Lodwar amewaondolea kodi ya nyumba wapangaji wake kwa mwezi mmoja katika juhudi za kuwapunguzia makali ya kiuchumi yanayotokana na virusi vya corona.
Akizungumza na meza yetu ya habari mjini Lodwar mmliliki wa nyumba hizo Justus Eleman amesema amechukua hatua hiyo kwa kuelewa matatizo wanayopitia wapangaji wake ambapo ametaka watumie pesa ambazo wangemlipa kwa mwezi mmoja kununua chakula kwa familia zao wakati huu mgumu
Aidha kutokana na kitendo hicho cha hisani, mfanyabiashara huyo anayemiliki nyumbani za makazi, atapoteza mapato takriban shillingi elfu 66 kwa mwezi
Kwa upande wao wapangaji wa nyumba hizo, wamesema tangazo la bwana Eleman limewapa afueni ikizingatiwa kuwa tangu virusi vya corona viingie nchini vibarua ambavyo wamekuwa wakitegemea kujikimu vimepungua.
Hata hivyo kitendo cha mfanyabiashara huyo kimewachangasha Wakenya wengi tuliozungumza nao ambapo wamewaomba wamiliki wa nyumba za kupanga maeneo mengine ya nchi waige mfano huo wa kutoa msamaha wa kodi wakati huu mgumu.