Ni vema mswada kuhusu watoto mwaka 2018 kutekelezwa kwa vitendo na kuwa sheria ili kuweka uzito na uhai kwa masuala yanayohusu mtoto.
Ndio wito wa watoto gatuzi la Pokot Magharibi katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto Mwafrika chini ya usimamizi wa mashirika ya Declairs, DSW, SIKOM na Idara ya Watoto chini ya Serikali kuu.
Katika mazungumzo na North Rift Radio Gavana wa watoto kaunti hiyo Mercyline Chebet amesisitiza umuhimu wa kupasishwa kwa mswada wa mwaka 2018 kuwa sheria ili kumpa mtoto sauti kando na kumuepusha na dhuluma.
Ni kuali ambayo imechachawizwa na Moses Kibet ambaye amependekeza viongozi kutilia maanani masuala ya watoto kuliko siasa ambazo hazina uzito kwenye mizani ya ukuwaji wa jamii yenye maadili na siha njema.