Naibu kamishna wa kaunti ndogo ya Marakwet Mashariki kaunti ya Elgeiyo Marakwet Simon Osumba ametoa wito kwa wazazi kuhakikisha wanawaelekeza wanao kwa njia bora kupitia mafunzo na mawaidha ili wasijihusishe na utovu wa nidhamu ambao umeendelea kushuhudiwa katika shule mbalimbali nchini
Akizungumza katika shule ya upili ya Kipkaner wakati wa ufunguzi wa madarasa yaliyojengwa kwa fedha za CDF, Osumba amesema wazazi wamewatelekeza wanao na hivyo kuchangia uozo katika jamii.