Rais Uhuru Kenyatta amezuia Mikusanyiko ya Kisiasa kwa siku 30 kuanzia Machi 12 ili kuzuia maambukizi ya Virusi vya Corona yanayoiandama nchi hiyo.
Zuio la kutotembea usiku limeongezwa kwa siku 60, ambapo amesema amechukua hatua hiyo kutokana na Wimbi la Tatu la Virusi vya Corona ambavyo wanakumbana navyo.
Kenyatta amesema Mikusanyiko ya Kisiasa inawaweka Wakenya kwenye hatari ya kupata maambukizi kwa kuwa watu hawawezi kuachiana nafasi.
Aidha amebainisha kuwa tangu wapigwe na COVID-19 wamepoteza takriban bilioni 560 za Kenya sawa na Tsh. Trillioni 11.8