Muungano wa Maafisa wa Kliniki nchini umetoa onyo kwa Waziri wa Afya Mutahi Kagwe kwamba utamchukulia hatua kali za kisheria kwa madai ya kusitisha marupurupu ya kufanya kazi katika mazingira magumu msimu huu wa janga la Corona.
Mwenyekiti wa Muungano huo Peterson Wachira amesema wanachama wake wataendelea na mgomo wao hadi pale magavana watakapowajibika na kuangazia lalama zao.
Aidha amesisitiza kwamba magavana wamekuwa kizingiti cha kuafikiwa kwa mwafaka kuwaruhusu wahudumu wa afya kurejea kazini.