Wahudumu wa boda boda kote nchini wanatarajiwa kupokea mafunzo kuhusu sheria za barabarani, ujuzi wa kuendesha pikipiki sawa na ujasiriamali katika biashara hiyo.
Mkurugenzi katika Mamlaka ya Usalama Barabarani NTSA Badu Katelo anasema mpango huo wa serikali unawalenga wanabodaboda takriban milioni 1.4 na utaendeshwa na shirika la huduma kwa vijana NTS kwa ushirikiano na ntsa, wizara ya usalama wa ndani pamoja na serikali ya kaunti.
Katelo amekariri kwamba sekta ya bodaboda imechangia pakubwa katika kuwaajiri vijana kando na kuchangia shilingi billion 350 kwa pato la taifa kila mwaka hivyo pana haja ya sera mwafaka kuwekwa ili kuboresha sekta hiyo.