Katibu wa Muungano wa Wauguzi Nchini Seth Panyako anasema ataendelea kuwa kiongozi wa muungano huo licha ya pingamizi kutoka kwa baadhi ya watu
Akizungumza baada ya kuchaguliwa kwa mara nyingine kama katibu wa chama hicho Panyako amewataka viongozi wa kisiasa kujitenga na maswala ya sekta ya afya akisema mwingilio wa wanasiasa kwenye sekta hiyo huenda ikahujumu juhudi za wahudumu wa afya kupata haki zao.