Serikali imefuta marufuku iliyoweka juu ya kuagiza Mahindi kutoka Uganda na Tanzania huku ikiambatanisha masharti kwenye uingizaji wa Zao hilo.
Mnamo Machi 5, Serikali ya Kenya iliweka marufuku ya kuingiza Mahindi yaliyoagizwa kutoka nje kwa lengo la kuzuia sumu inayosababisha Saratani kwa binadamu.
Moja ya sharti lililowekwa ni washikadau wote wanaoshughulika na uagizaji wa Mahindi watahitajika kusajiliwa, shehena zinazoingia lazima zifuatwe na cheti cha viwango vya Aflatoxin na Wafanyabiashara wanapaswa kutoa maelezo ya maghala yao.
Cheti kinapaswa kuonesha kwamba viwango vya Aflatoxin vinazingatia kiwango cha juu kinachohitajika cha sehemu 10 kwa bilioni.