Kiongozi wa Chama cha ODM Raila Odinga amelazwa Hospitali ya Nairobi kutokana na kuwa na uchovu wa mwili na maumivu makali.
Kaka wa Odinga, Oburu Odinga amesema ndugu yake haijaonesha dalili za Magonjwa ya Mfumo wa Hewa na hadi wameondoka Hospitali majibu ya COVID-19 yalikuwa bado hayajatoka.
Amesema kuwa hakuna haja ya kuhuzunika kutokana na Raila kuugua kwa kuwa kila mtu anaugua.