Rais Uhuru Kenyata mapema leo amezindua rasmi shughuli ya usambazaji wa chanjo dhidi ya virusi vya Corona hadi katika maeneo mbalimbali nchini
Akizungunza katika eneo la Kitengela ambapo chanjo hiyo imehifadhiwa rais Kenyata anasema ana imani kwamba wakenya wote watapata chanjo hiyo kusaidia kukabili ugonjwa wa COVID-19.
Aidha kiongozi wa taifa amewaonya Wakenya dhidi ya kupuuza masharti yaliyowekwa huku akiwataka kuendelea kuchukua tahadhari ili kuepuka Corona.
Kwa upande wake waziri wa Afya Mutahi Kagwe anasema uwepo wa chanjo hiyo hapa nchini ni hatua kubwa ikizingatiwa kwamba Kenya ni miongoni mwa mataifa ya kwanza barani afrika kupata chanjo ya kubali Corona.