Bunge la Kitaifa linatarajia kujadili Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Makosa Mtandaoni ambapo kama utapitishwa, Mtu atafungwa miaka 25 Jela au faini ya Ksh. Milioni 20 endapo atasambaza maudhui ya ngono mtandaoni.
Vivyo hivyo, Muswada huo unataka kuzuia utumiaji wa Vifaa vya Elektroniki katika kusambaza jumbe zinazochochea Ugaidi, Itikadi Kali za Kidini au Ibada.
Katika kurekebisha Sheria ya Uhalifu wa Mtandaoni, Muswada unasema Mtu ambaye atachapisha au kusambaza ujumbe unaochochea watu kujiunga au kushiriki katika shughuli za kigaidi, atahukumiwa faini isiyozidi Ksh. Milioni 5 au atakabiliwa na kifungo cha miaka 10 jela au vyote viwili