SERIKALI IMETOA HAKIKISHO KWA WAKULIMA KWAMBA NZIGE WA JANGWANI WATAKABILIWA VILIVYO.

You are currently viewing SERIKALI IMETOA HAKIKISHO KWA WAKULIMA KWAMBA NZIGE WA JANGWANI WATAKABILIWA VILIVYO.

Serikali imewaondolea Wakulima nchini wasiwasi wa mimea yao kuvamiwa na Nzige wa jangwani walioripotiwa kuingia Nchini kutoka taifa jirani la Somalia.

Msemaji wa Serikali kanali mstaafu Cyrus Oguna anasema Serikali imekabiliana vilivyo na Nzige hao waharibifu na mikakati kabambe imewekwa kuhakiksha kwamba wanamaliza kabisa wadudu hao ili wasisambae katika maeneo yote nchini.

Aidha Oguna ametaka wakenya kupiga ripoti kwa maafisa wa Serikali nyanjani panaporipotiwa uwepo wa Nzige hao ili hatua za dharura zichukuliwe. 

Alex Toilem

Mwandishi, mhariri na msomaji wa habari Northrift Radio 104.9/104.5FM kapenguria.