GAVANA WA KAUNTI YA NAKURU LEE KINYANJUI ASIFIA RUZUKU YA MAGARI KWA WAWAKILISHI WA WADI

You are currently viewing GAVANA WA KAUNTI YA NAKURU LEE KINYANJUI ASIFIA RUZUKU YA MAGARI KWA WAWAKILISHI WA WADI

Gavana wa Kaunti ya Nakuru Lee Kinyanjui ameunga mkono uamuzi wa Tume ya kuratibu mishahara ya wafanyikazi wa umma SRC kuwapa ruzuku ya magari Wawakilishi Wadi kote Nchini.

Kinyanjui anasema Wawakilishi Wadi sasa watakuwa wanatekeleza wajibu wao ikizingatiwa kwamba wana chombo cha kusafiria mashinani.

Kuhusiana na mswada wa marekebisho ya Katiba BBI, Kinyanjui anasema mabadiliko ya katiba kupitia mchakato wa BBI unafaa kutofautishwa na siasa za urithi za Mwaka wa 2022 akisema mapendekezo ya BBI yanalenga kumnufaisha mwananchi moja kwa moja.

Wakati huo huo ameshabikia kubuniwa kwa hazina ya ustawi ya wadi, kuongezwa kwa pesa za basari, mpango wa amani na utangamano wa itaifa kando na mapendekezo ya jinsi ya kukabili ufisadi ambayo yamejumuishwa ndani ya BBI.

Alex Toilem

Mwandishi, mhariri na msomaji wa habari Northrift Radio 104.9/104.5FM kapenguria.