Msemaji wa serikali kanali mstaafu Cyrus Oguna amewaonya wakenya dhidi ya kutapeliwa kulipia ada ili kupata kadi zao za huduma namba kwani hakuna ada yoyote inayotozwa wananchi kupokea kadi hizo.
Oguna amesema zoezi la kusambaza kadi hizo imeanza rasmi ambapo watu wazima watakabidhiwa kadi hizo huku watoto walio chini ya umri wa miaka kumi na nane wakipewa nambari maalum.
Aidha amedokeza kuwa watu 37,000 walisajiliwa katika awamu ya kwanza ya mpango wa huduma namba huku wengine wakitarajiwa kusajiliwa mwezi Aprili mwaka huu.