Ushindi wa Peter Navulondo wa chama cha ANC katika eneo bunge la Matungu umeonyesha dhahiri kwamba eneo la Magharibi limeungana.
Ndio kauli ya Kinara wa chama cha ANC Musalia Mudavadi anayesema kwamba wataungana na kiongozi wa FORD Kenya Moses Wetangula pamoja na viongozi wengine kuhakikisha kwamba eneo la Magharibi linaungana na kusalia imara kuelekea uchaguzi mkuu mwaka ujao wa 2022
Aidha Mudavadi anasema sasa ni wakati wa vyama vingine vya kisiasa sawa na viongozi wao kuwaunga mkono viongozi wa Magharibi ya nchi kwenye azma yao ya kuongoza taifa la kenya kupitia kiti cha urais.